Monday, 10 August 2020

KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

 

KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

Ni degedege inayomkuta mama mjamzito au mara baada ya kujifungua nayo husababishwa na uwepo wa mimba!

Ni ugonjwa namba 2 kusababisha vifo vinavyotokana na uzazi(maternal death), hivyo ni tatizo muhimu sana kulifahamu japo kwa muhtasari.


NINI HASA HUSABABISHA KIFAFA CHA MIMBA?

Haijulikani hasa kuwa nini chanzo cha hili tatizo ijapokua kuna nadharia zinazotumika kuelezea kutokea kwake.


VIPI VIHATARISHI VYA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kushika mimba kwa mara ya kwanza ( primegravida).

2.kuwa na tatizo la shinikizo la damu kabla ya ujauzito

3.kuwa na mimba zaid ya mtoto 1,mapacha( multiple pregnancy)

4. Kubadili mume( hii ni kwa wale waliokwisazaa #multigravida#) wana hatari ya kupata kifafa cha mimba kama ujauzito umepata kwa mume ambaye si yule  mwenye ujauzito wa kwanza (changing husband)

5.Historia ya kifafa cha mimba kwa mama wa mumeo( yaani kama mkweo alipata kifafa cha mimba nawe unahatari ya kupata)

6.kushika mimba ya kwanza umri wa zaid ya miaka 35, n.k


DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA

1. Degedege(convulsion) nayo iambatane na:-

----- Protein ktk mkojo.

-----Shinikizo la daumu(yaani zaid au sawa na 140/90mmhg

NB: Hata shinikizo la damu chini ya 140/90mmhg anaweza apate degedege.


Dalili Tanguliza Kabla ya Kifafa Cha Mimba

-kuumwa sana na kichwa(severe headache)

-kuona giza au kutoona vizuri(blurred vision)

- Maumivu sehemu ya juu ya tumbo(epigastric pain) #wanaita chembe ya moyo#


Dalili hzi zikimkuta mama mjamzito mwenye shinikizo la damu na protein kwenye mkojo zinaashiria ana hatari ya kupata kifafa cha mimba muda wowote.


WAKATI GANI HASA HUTOKEA KIFAFA CHA MIMBA?

Mara nyingi hutokea kwa mimba yenye umri wa wiki 20 na zaidi, na inaweza itokee wakati wa ujauzito au mara tu baada ya kujifungua!


MATIBABU

-Hii ni dharura (emmergency), madaktari na manesi watakusanyika kitimu kumhudumia mgonjwa.

-Baada ya kuisha degedege,na kupatiwa dawa za presha, mama ataanzishiwa dawa za uchungu hata kama mimba ilikua bado hajafikia umri wa kujifungua, kwa kuwa katika hali hii wanaokoa maisha ya mama kwanza(mother's life first). Anaweza afanyiwe upasuaji wa kuzaa kama patakua na uhitaji huo.


MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kupoteza maisha ya mama(MATERNAL DEATH)

2.Kupoteza maisha ya mtoto(IUFD)

3.mama anaweza kupata upofu(Blindness)

4. Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi(Renal failure)

5.Ini linaweza kushindwa kufanya kazi(liver failure).

6. Shida ktk ubongo N.K


KUJIKINGA

Kuhudhuria cliniki na huko hakikisha unapimwa presha na mkojo  kila uhudhuriapo clinic.

Ukigundulika mapema una pressure utahudumiwa kwa taadhari na kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha hupati kifafa cha mimba au pale dalili zikigundulika maamuzi yafanyike kwa wakati.

Kwa waliogundulika na presha ya ujauzito (Pregnancy induced hypertensio), presha ya siku nyingi na ujauzito atumie dawa ipasayo kama alivyoelekezwa na daktari.


Dr.ONESMO EDISON

0759913570

onesmo999@gmail.com

Wednesday, 19 December 2018

HAYA NDIYO MADHARA YA TABIA YA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI

Kunyonya sehemu za siri ni tabia ambayo huweza kukuweka hatari kupata magojwa. 90% ya vijana wakitanzania walishawahi kunyonya uume au uuke ndani ya maisha yao.

herpes simplex ndio ugojwa ambao mara nyingi mtu hupata wakati wa kuyonya sehemu zasiri.kuna aina mbili za ugojwa huu, kuna herpes simplex type 1 and herpes simplex tpye 2.

HAYA NDIO MADHARA KUMI YA KUPIGA PUNYETO…..{ MASTURBATION}



Punyeto ni nini?
Hii ni tabia ambayo mwanamke au mwanaume anajichua sehemu za siri ili kufika kileleni, mara nyingi kitendo hiki hufanyika na muhusika akiwa peke yake chumbani au bafuni.
Wahanga wengi wa tabia hii ni wanaume kwani huanza katika umri mdogo sana kwasababu ya uoga wa kufuata wasichana na kuangalia video za ngono ambazo huwasukuma kufanya vitendo hivi..

UNAJUA KWANINI WANAWAKE WAKO HATARINI ZAIDI KUPATA MAABUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KULIKO WANAUME.



Wanawake wako hatari zaidi kuliko wanaume kupata maabukizi ya virusi vya ukimwi kwa sababu:

1. Bao/shahawa za mwanaume hukaa ndani ya uke wa mwanake kwa masaa 72.

2. aina ya ngozi(vaginal mucosal) ambayo iko ndani ya uke mwanamke ninyepesi sana kuchubuka ukilinganisha naya ngozi iliopo kwa mwanaume.

Tuesday, 18 December 2018

HIZI NDIO SABABU 17 KWANINI UFANYE TENDO LA NDOA



Tendo la ndo nikitu muhimu sana ndani ya mahusiano. Nimuhum sana kuliko unavo fikiria wewe. Hisia zako zina lisha nafsi yako,chakula kitaweka mwili wako ufanye kazi kama kawaida.
Lakini tendo la ndoa nikitu ambayo kinalisha nafsi pamoja na mwili kwa wakati mmoja.

Wednesday, 23 December 2015

ZIFAHAM FAIDA ZA KUYONYESHA MTOTO KWA MAMA NA MTOTO MWEYEWE.NA JINSI YA KUNYOYESHA.


kunyoyeshwa kwa mtoto vyakutosheleza ndio msingi wa afya bora ya mtoto. kunyoyesha mtoto kwa uzembe huweza kumuweka mtoto hatarini kupata matatizo ambayo huweza kumsumbua maisha yake yote.

Wednesday, 11 November 2015

FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU SHINIKIZO LA DAMU (Muuaji wa Kimya Kimya)


Kama tatizo la shinikizo la damu au presha halipatiwi tiba huweza kuleta matatizo au maafa kama ugonjwa wa moyo, kufa kwa figo, kupooza, upofu, au athari katika ubongo.

Shinikizo la damu ni neno la kiganga linalotumika kuelezea hali ya ugonjwa wa shindikizo la juu wa damu. Shinikizo la damu ni muhimu kwa ajili ya kusaidia kusukuma damu katika sehemu zote za mwili, lakini shinikizo la damu la juu linaweza kuleta madhara ya kiafya na huweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.