Monday, 10 August 2020

KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

 

KIFAFA CHA MIMBA (ECLAMPSIA)

Ni degedege inayomkuta mama mjamzito au mara baada ya kujifungua nayo husababishwa na uwepo wa mimba!

Ni ugonjwa namba 2 kusababisha vifo vinavyotokana na uzazi(maternal death), hivyo ni tatizo muhimu sana kulifahamu japo kwa muhtasari.


NINI HASA HUSABABISHA KIFAFA CHA MIMBA?

Haijulikani hasa kuwa nini chanzo cha hili tatizo ijapokua kuna nadharia zinazotumika kuelezea kutokea kwake.


VIPI VIHATARISHI VYA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kushika mimba kwa mara ya kwanza ( primegravida).

2.kuwa na tatizo la shinikizo la damu kabla ya ujauzito

3.kuwa na mimba zaid ya mtoto 1,mapacha( multiple pregnancy)

4. Kubadili mume( hii ni kwa wale waliokwisazaa #multigravida#) wana hatari ya kupata kifafa cha mimba kama ujauzito umepata kwa mume ambaye si yule  mwenye ujauzito wa kwanza (changing husband)

5.Historia ya kifafa cha mimba kwa mama wa mumeo( yaani kama mkweo alipata kifafa cha mimba nawe unahatari ya kupata)

6.kushika mimba ya kwanza umri wa zaid ya miaka 35, n.k


DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA

1. Degedege(convulsion) nayo iambatane na:-

----- Protein ktk mkojo.

-----Shinikizo la daumu(yaani zaid au sawa na 140/90mmhg

NB: Hata shinikizo la damu chini ya 140/90mmhg anaweza apate degedege.


Dalili Tanguliza Kabla ya Kifafa Cha Mimba

-kuumwa sana na kichwa(severe headache)

-kuona giza au kutoona vizuri(blurred vision)

- Maumivu sehemu ya juu ya tumbo(epigastric pain) #wanaita chembe ya moyo#


Dalili hzi zikimkuta mama mjamzito mwenye shinikizo la damu na protein kwenye mkojo zinaashiria ana hatari ya kupata kifafa cha mimba muda wowote.


WAKATI GANI HASA HUTOKEA KIFAFA CHA MIMBA?

Mara nyingi hutokea kwa mimba yenye umri wa wiki 20 na zaidi, na inaweza itokee wakati wa ujauzito au mara tu baada ya kujifungua!


MATIBABU

-Hii ni dharura (emmergency), madaktari na manesi watakusanyika kitimu kumhudumia mgonjwa.

-Baada ya kuisha degedege,na kupatiwa dawa za presha, mama ataanzishiwa dawa za uchungu hata kama mimba ilikua bado hajafikia umri wa kujifungua, kwa kuwa katika hali hii wanaokoa maisha ya mama kwanza(mother's life first). Anaweza afanyiwe upasuaji wa kuzaa kama patakua na uhitaji huo.


MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA

1.Kupoteza maisha ya mama(MATERNAL DEATH)

2.Kupoteza maisha ya mtoto(IUFD)

3.mama anaweza kupata upofu(Blindness)

4. Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi(Renal failure)

5.Ini linaweza kushindwa kufanya kazi(liver failure).

6. Shida ktk ubongo N.K


KUJIKINGA

Kuhudhuria cliniki na huko hakikisha unapimwa presha na mkojo  kila uhudhuriapo clinic.

Ukigundulika mapema una pressure utahudumiwa kwa taadhari na kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha hupati kifafa cha mimba au pale dalili zikigundulika maamuzi yafanyike kwa wakati.

Kwa waliogundulika na presha ya ujauzito (Pregnancy induced hypertensio), presha ya siku nyingi na ujauzito atumie dawa ipasayo kama alivyoelekezwa na daktari.


Dr.ONESMO EDISON

0759913570

onesmo999@gmail.com

No comments:

Post a Comment