Sunday, 1 November 2015

FAHAMU KUHUSU UVIMBE WA SEHEMU YA HAJA KUBWA.(HAEMORRHOIDS)


HAEMORRHOIDS

Huu ni ugojwaa mbao una asili sehemu ya haja kubwa ya binadamu. Mishipa ya damu inayo sambaza damu katika sehemu ya haja kubwa huvimba.

VISABABISHI
  1. Unene ulio pitiliza.
  2. kuogezeka kwa pressure ya damu katika sehemu ya haja kubwa.
  3. Kusukuma mkojo kwanguvu kubwa sana huweza sababisha hili tatizo
  4. Upungufu wa misuli ya sehemu ya  haja kubwa.
  5. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
  6. Ujauzito huweza kumuweka mwanamke hatarini kupata hili tatizo
  7. Choo huwa kigumu sana, huweza sababisha mishipa ya damu kuvimba katika sehemu ya haja kubwa.

KUNA AINA MBILI ZA UGONJWA HUU
  • Haemorrhoid za ndani.( internal haemoroids.)
  • Haemorrhoid za nje.(External haemorroids.)

Haemorrhoid za nje.(external haemorroids)
Hizi hutokea kwa nje katika sehemu ya haja kubwa, kuna kipindi hizi zaweza kua na maumivu makali na uvimbe nje ya sehemu ya haja kubwa.
Uvimbe huu huweza kua unawasha mara kwamara
Haemorrhoids za ndani.( internal haemorroids)
Hizi zimegawanyika katika sehemu nne
  • hatua ya kwanza - haemorrhoids hazichomozi
  • hatua ya pili -uvimbe ule hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe.
  • hatua ya tatu- uvimbe huchomoza wakati wa haja kubwa na hurudi yenyewe.  
  • hatua ya nne -uvimbe huchomoza wakati wowote.

Dalili za ugonjwa huu
  1. Hujisikia kama vile kuna kitu kina chomoza sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisaidia.
  2. Kuvuja kwa damu katika sehemu ya haja kubwa

 dr onesmo edison
0759913570
0673913571




No comments:

Post a Comment