Uzazi wa mpango ni aina ya uzazi ambao hutumiwa kuzuia mimba zisizotarajiwa. Njia zote za uzazi wa mpango huzuia mbegu za mwanamume kwenda kukutana na yai la mwanamke. Kuna aina mbalimbali za uzazi wa mpango ambazo ufanyika kwa njia tofauti.
njiti.
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.
njia hii ni bora kuliko zote?
kwanini kijiti
kama unatumia kijiti hata kama kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata mtoto.
ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.kijiti hufanya kazi kwa mda mrefu,haiongezi uzito
muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa
-Kizuizi: Inazuia mbegu za kiume zisikutane na ovari ama yai mfano:
1. Kondomu ya kiume
- Huu ni mpira laini ambao mwanamume huuvaa kwenye uume wakati anapotaka kufanya ngono.
- Mpira huu uzuia mbegu za kiume kutoka kwa mwanamume kwenda kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke wakati wakifanya ngono.
- Mpira huu pia hutumika kumlinda mtu dhidi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono.
- Kondomu huvaliwa kwenye uume uliosimama kabla ya kujamiiana.
- Kondomu ni lazima itumike mara moja tu.
- Kondomu inakuwa nzuri tu utakapoitumia kwa usahii na mara kwa mara.
2. Kondomu za kike
- Hii ni plastiki nyembamba sana ambayo huingizwa ndani ya uke wa mwanamke kabla ya kujamiiana. Kama ilivyo kondomu ya kiume na hii pia uzuia mbegu za kiume kwenda ndani ya mfuko wakizazi wa mwanamke.
- Mbali na kazi hiyo pia hutumika kuzuia mimba, VVU na magonjwa mengine ya ngono. Ni lazima itumike moja kwa kila tendo na isitudiwe.
- Kondomu za kike zinapatikana katika zahanati na maduka ya dawa.
- Homona: Njia hii ina kazi ya kuzuia kukomaa yai katika mfuko wa uzazi wamwanamke.
Mfano:
1 . Vidonge vya Uzazi wa mpango
- Mwanamke ana homoni ambazo husababisha mfuko wake wa uzazi kutoa yai kila mwezi. Uzazi wa mpango wa kutumia kidonge huufanya mfuko wa uzazi kuacha kufanya hivyo.
- Mwanamke lazima ameze kidonge kimoja kila siku. Kama atasahau kumeza kidonge na kisha akafanya ngono anaweza kupata ujauzito.
- Vidonge vya uzazi wa mpango uzuia mimba lakini si VVU na magonjwa mengine ya ngono.
2. Sindano za Uzazi wa Mpango
- Sindano za uzazi wa mpango hutolewa kwa wanawake tu.
- Zenyewe zina uwezo wakuzuia yai kufikia mfuko wa uzazi kila mwezi.
- Wanawake huchomwa sindano kila baada ya wiki 6-12.
- Sindano huzuia mimba, lakini haina uwezo kuzuia magonjwa ya ngono kama VVU.
-Uzazi wa mpango wa kutumia kifaa cha Intrauterine (IUD): Kifaa hiki kina kazi ya kuzuia uzalishaji wa virutubisho wa yai au mayai katika mfuko wa uzazi / mimba
Mfano:
1.Kifaa cha IUD cha kitanzi
- Kitanzi ni kipande cha plastiki laini ambacho kimezungushwa kwenye waya wa shaba. Kifaa hiki huingizwa katika mfuko wa uzazi na daktari kwa kutumia chombo maalum. Kinaweza kukaa huko kwa muda wa miaka mitano na kuondolewa na daktari. Kifaa hiki kina kazi ya kuzuia yai lisiingie kwenye mfuko wa uzazi.
- Hata hivyo kifaa hiki hakifai kwa wasichana wadogo kutokana na kwamba kinaweza kumsababishia madhara na hata utasa.
- Kifaa hiki cha IUD pia hakina uwezo wa kuzuia magonjwa ya ngono kama VVU.
-Njia ya Kudumu – Njia hii ina kazi ya kuzuia mbegu za kiume zisikutane na yai la mwanamke.
Mfano:
Kufunga kizazi
- Njia hii kazi yake kuzuia mimba milele.
- Mwanamume anaweza kufanyiwa upasuaji ili kuzuia mbegu kutoka kwenye mfuko wa uzazi na kuufikia yai.
- Kwa upande wa mwanamke anaweza kufanyiwa upasuaji wakuzuia mrija wa kusafirisha mayai ili yasifikie mfuko wa uzazi.
- Shughuli hizi kwa kawaida hufanyiwa wanaume au wanawake wenye umri zaidi ya miaka 30 ambao hawataki kuwa na watoto zaidi.
- Njia hii pia haina uwezo wa kuzuia VVU.
DR ONESMO EDISON
0759913570
0673913571
No comments:
Post a Comment