Sunday, 25 October 2015

FAHAM JINSI YA KUMYONYESHA MTOTO.


wamama wengi sana hukosea wakati wa kuwayonyeshwa watoto wao. mama anazania mtoto ameshimba kumbe tumbo la mtoto linakua limejaa gesi tu.
hapa ndipo umuhimu wa mwanamke kuhuzulia clinic kipindi akiwa mjamzito unakuja. wanawake wajawazito hufudishwa namna ya kuyonyesha.

Friday, 23 October 2015

FAHAM KWA UNDANI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA ZAKE.




Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila

Thursday, 22 October 2015

KAMA WEWE NI MWANAMKE HIKI KITABU KINA KUHUSU.JUA AFYA YA MWANAMKE..



sababu nyingi sana zinaweza kuchangia kupungua kwa nguvu za misuli ya uke na na tumbo la chini kwa ujumla ikiwemo ujauzito, umri mkubwa, kuzaa watoto, upasuaji na kua na uzito mkubwa.
Wanawake wengi ambao wana misuli iliyolegea hawafiki kileleni kirahisi wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine huhitaji uume mnene ili kusugua mishipa yao ya

Tuesday, 20 October 2015

NINI HUSABABISHA KOLODANI KUVIMBA.



Magojwa tofauti huweza kusababisha kolodani kuvimba, kuvimba kwa kolodani huweza kugawanywa katika sehem mbili.

Sababu ya kuvimba inakua nje ya kolodani.
-Inguinal hernia
-Enlarged inguinal lymph node kuvimba kwa mtoki

Monday, 19 October 2015

UKIONA DALILI/MAGOJWA HAYA KAPIME VIRUSI VYA UKIMWI.


Maabukizi ya virusi vya ukimwi yamekua tatizo kubwa sana kwa jamii yetu tunayo ishi. Wagojwa wa kwanza wa virusi vya ukimwi waligundilika mwaka 1983 na walikua wa tatu tu. Kufika mwaka 2012 kati ya wagojwa 1.3-1.5 milioni wali lipotiwa kupatikana na virusi vya ukimwi na 450,000 kati ya hao kuhitaji dawa za kurefusha  maisha. ARV(30%).

Sunday, 18 October 2015

ZIFAHAM NJIA TOFAUTI ZA UZAZI WA MPANGO NA IPI NZURI KULIKO ZOTE.


Uzazi wa mpango ni aina ya uzazi ambao hutumiwa kuzuia mimba zisizotarajiwa. Njia zote za uzazi wa mpango huzuia mbegu za mwanamume kwenda kukutana na yai la mwanamke. Kuna aina mbalimbali za uzazi wa mpango ambazo ufanyika kwa njia tofauti.
Ni aina ngapi za uzazi wa mpango?

VIRUTUBISHO VYA MULTI MACA NAMAAJABU YAKE KWEYE KUTIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA UZAZI KWA WANAWAKE NA WANAUME.




ukisoma historia ya dunia, miaka 2000 iliyopita huko nchi ya peru ya marekani ya kusini, wanawake na wanaume walikua wakitumia mzizi huu kwa matibabu mbalimbali ya kibinadamu kama kuishiwa nguvu za kiume na kuwezesha wanawake kuzaa mpaka miaka zaidi ya arobaini bila shida. lakini pia kuwasaidia walioshindwa kuzaa sababu ya shida ya uzazi..

Saturday, 17 October 2015

ZIFAHAM DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.


Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma.
Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba.
Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu, tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina.
Saratani ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu, anaachana naye anaishi na mwingine, yaani mara kwa mara hana msimamo, anabadilibadili wanaume, wanawake wanaofanya ngono na wanaume wasiofanyiwa tohara pia hupatwa na tatizo hili la saratani ya shingo ya uzazi.
Saratani ya shingo ya uzazi pamoja na kuchangiwa na mambo yote hayo hapo juu, husababishwa hasa na kirusi kiitwacho ‘Human Papilloma virus’ au kwa kifupi ‘HPV’. Kirusi hiki huenezwa kwa njia ya ngono, mwanaume huwa hakimuathiri bali yeye hukibeba na kukisambaza kwa wanawake kwa hiyo mwanamke anayechanganya wanaume hajui wapi atakipata.

Ukubwa wa tatizo
Saratani ya shingo ya kizazi ina tabia ya kusambaa endapo haitagundulika na tiba haitafanyika mapema. Saratani husambaa katika kizazi, nyonga hadi katika mapafu. Ikishambulia nyonga, mwanamke hulalamika maumivu chini ya tumbo.
Saratani hii ina tabia ya kusambaa kwa kasi na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa  husababisha kifo kwa mwanamke. Saratani huwa haiambukizi.

Dalili za awali za saratani ya shingo ya uzazi
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni na muwasho mara kwa mara. Tatizo hili hutibiwa na kujirudia tena mara kwa mara.
Mwanamke hulalamika kwamba ametibiwa sana kwa dawa za kumeza na kuingia ukeni lakini hapati nafuu. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwishowe hutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa.
Saratani inaposambaa na kushambulia shingo ya uzazi huathiri ukeni na kuumiza njia ya mkojo na kibofu.
Uke huvimba na kuonekana kuziba na mlango wa kizazi au ngozi ya ndani ya ukeni ikiguswa tu kidogo basi hutokwa na damu kwani huwa laini sana. Hii ni hatua mbaya na ya mwisho katika saratani inaposambaa.

Uchunguzi
Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi hufanyika katika vituo mbalimbali katika kampeni maalum dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.
Uchunguzi pia hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya katika kliniki za magonjwa ya kinamama ambapo vipimo mbalimbali  hufanyika mojawapo ikiwa ni kuangalia mlango na shingo ya uzazi.
Kipimo cha Ultrasound pia kitafanyika kuangalia athari katika kizazi. Majimaji ya ukeni yatapimwa kuangalia maambukizi na uchunguzi wa awali wa saratani utafanyika.
Endapo mlango wa uzazi utakuwa umeathirika sana, basi kinyama kitatolewa na kupimwa katika maabara kubwa kuthibitisha tatizo.

Ushauri
Ni vema mwanamke yeyote anayejihisi maumivu chini ya tumbo na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho uwepo au usiwepo awahi hospitali kwa uchunguzi. Waone madaktari wa kinamama kwa uchunguzi sahihi katika hospitali za mikoa.

HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE KUKOSA HEDHI.


Wengi wanafahamu kwamba mwanamke akipata mimba hawezi kuziona siku zake za hedhi bila kujua kuwa ziko sababu nyingine zinazoweza kusababisha jambo hilo. Kwa kawaida mwanamke huacha kupata hedhi kitaalam huitwa Menopause anapofikisha umri wa miaka 42 -55 na kuendelea.
Leo nitazieleza sababu nje ya utaratibu huo wa kimaumbile unaoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).

MAABUKIZI YA WADUDU.
Maabukizi ya magojwa tofauti yaweza sababisha mwanamke asipate kuona siku zake.magojwa yale yana vuruga mfumo wa utoaji wa hormone katika mwili wa mwanamke. eg PID (pelvic inflamatory disease, gono etc
SIGARA Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.
 UNENE Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.Kitaalam hali hiyo inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani Sex homones.
ULEVI Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku.
KUTOKULA NYAMA Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao wamo katika hatari ya kukosa kuona siku zao za hedhi. Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari ya kupata saratani ya matiti. Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiiana kwa mwanamke. Hali hiyo husababisha tupu za mwanamke kuwa kavu, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
 USHAURI Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka ni vyema akaenda kumuona daktari ili afanyiwe uchunguzi na kama ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi.
Dr Onesmo Edison
0759913570
0673913571

FAHAM YOTE KUHUSU HEDHI.



HEDHI   ni mabadiliko ya mpangilio yanayo tokea ndani ya mfumo wa uzazi na mayai ya mwanamke. mzuguluko huu unahitajika kwajili ya kuzalisha mayai na kuweza kuandaa mfuko wa uzazi kwajili ya mimba.
hadi 80% ya wanawake hupata dalili tofauti siku moja au mbili kabla ya hedhi.
dalili kama
1. chunusi
2. maumivu katika matiti.
3. uchovu
4. hubadilika kwa mood.
hedhi ya kwanza huanza kati ya miaka 12-15 miaka. wakati unai itwa menarch kitaalam.wengine kuanza mapema mpaka miaka 8.

urefu wa hedhi moja una wastani ya siku 21-45 katiak wanawake wadogo na 21-31 katika wanawake wazima.hedhi huacha kutokea katika miaka 45-55.

wanawake tofauti huvuja dam kati ya siku 2-7

yote tajwa hapo juu huedeshwa na hormone. kila mzunguko mmoja umegawanyika katika sehem tatu ndani ya mayai na mfuko wa uzazi.1) menstruation 2) proliferation phase 3) secrectory phase.

Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. 

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka  sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.

Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku  28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.

Kama mzunguko wako ni mrefu labda  siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.


Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
mwisho: maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka  ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike.


DR ONESMO EDISON
0759913570
0673913571

Thursday, 15 October 2015

KAMA WEWE MWANAUME UNA TATIZO LA KUFIKA KILELENI HARAKA KABLA MPENZI WAKO HAJARIDHIKA SOMA HAPA

 
Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.
Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.
Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}
Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.
  • ·         Kupiga punyeto haraka kipindi  cha kubalehe kuogopa kukutwa na watu.
  • ·         Kukaa mda mrefu sana bila  kushiriki tendo la ngono.
  • ·         Kuwa na wasiwasi kipindi cha  tendo la ndoa kwamba huenda mwanamke anaweza akavaa akaondoka kabla hujaridhika.
  • ·         Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya  fahamu.
  • ·         Kurithi tatizo kwenye ukoo. I;e genetically inherited.
  • ·         Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.
Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
   
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.
·         Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}:  matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.
·         Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.
Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
·         Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.
·         Kandamiza perineum kwa kidole:Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka
.
·         Punguza wasiwasi: hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu,  hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.
·         Fanya taratibu: picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama bata. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.
·         Badilisha style: ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.
·         Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa
·         Toa mawazo kwamba unafanya ngono: hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.
·         Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.
·         Kandamiza sehemu ya shingo la uume: hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

tumia kilevi: unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume au bia moja kwa siku kwa wanawake unasidia sana mfumo wa moyo lakini sio bia tu hata wine, whisky au kilevi chochote kwa kiwango kidogo kama glass moja kwa siku..pamoja na faida ya moyo, pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.
·      
Matibabu ya kutumia dawa.
1.       Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na  clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia mara 20 zaidi kutoa mbegu zikitumika vizuri.
2.       anesthetic creams:  hii ni dawa zinazopakwa kwenye kichwa cha uume kuzuia msisimko kipindi cha tendo hilo mfano lidocaine cream.. 

mwisho: shida hii inaathiri sana watu wanokaa muda mrefu sana bila kushiriki kingono, nakushauri utumie pombe au dawa kama ukijikuta umekaa mda mrefu sana bila kushiriki ngono lakini kama hua unalala na mwanamke angalau mara nne kwa wiki huhitaji dawa wala pombe kwani tatizo kwako litapungua sana...
 
DR EDISON ONESMO
0759913570
0673913571

HAYO NDIO MAMBO KUMI YA SIRI AMBAYO HAYASEMWI KUHUSU JUISI ZA ALOE VERA.



Aloe vera sio mmea mpya masikioni mwa watu kwani umetumika kwa miaka mingi sasa kutibu magonjwa mbalimbali na kuzuia vifo vingi ambavyo vingesababishwa na magonjwa mbalimbali. huku kwetu afrika watu wanafikiri bidhaa zinazotokana na mmea huu adimu ni dawa tu kwa binadamu. lakini ni kosa kusema hivyo kwani dawa ni kitu ambacho ukitumia kinakutibu na kuacha baadhi ya sumu zake...lakini bidhaa za mmea huu ni virutubisho ambavyo vinakutibu na kukuzuia na magonjwa mbalimbali. kiufupi wenzetu huko nje wanatumia bidhaa hii kama sehemu ya chakula lakini sisi tunatumia tukiugua tu, huenda ni sababu ya ugumu wa maisha yetu lakini kama unaweza bidhaa hizi zisiishe ndani kwako.
leo naomba nikupe siri kumi kumi usizozijua za  juice hii inayotokana na mmea wa alo evera ikiwa imetengenezwa bila kuwekewa kemikali hata moja.

kuondoa sumu mwilini: kama umeshawahi kuona mmea wa aloe vera yale maji yake ya ndani  ni mazito kama mlenda hivi, kwa hiyo ukinywa juice yake haitoki haraka tumboni kama maji ya kawaida hivyo kutoka kwake taratibu kunaifanya inyonye sumu zilizoko kwenye mfumo wa chakula  na mfumo wa damu ili kutoka nazo nje na kukuacha mpya.

hupunguza uzito; kuondoa sumu mwilini ni sawa na kufuta baadhi ya faili kwenye computer iliyojaa kwani computer hiyo itaanza kufanya kazi kwa haraka sana, hivyohivyo kwenye mwili sumu zikitoka mwili hufanya kazi kwa haraka sana na kupunguza mafuta yaliokua yameuelemea.

hulainisha choo; mara nyingi watu hupata choo ngumu sana kwa sababu ya kula vyakula visivyo na maji ya kutosha kama nyama nyingi na wanga bila kula matunda hivyo juice hii hulainisha na kusafisha njia ya choo kubwa, hii itakusaidia kupata choo kilaini sana.

ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari; kama unasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari juice ya aloe vera inasaidia sana kushusha sukari ya mwili na kukufanya uishi maisha safi sana.

matibabu ya magonjwa ya kinywa; utafiti unaonyesha juice hii huua bacteria wa mdomoni ambao huweza kusababisha magonjwa ya meno na ndio maana kuna dawa za meno zinatengenezwa kwa mmea huu.

hutibu magonjwa ya ngozi na chunusi; juice hii huupa mwili kiwango cha madini na vitamini za kutosha pia kuongeza maji mwilini, hii hulainisha ngozi yako na kukufanya ue na ngozi laini sana na yenye afya.

huongeza urefu wa nywele; kama unataka kua na nywele ndefu hasa kwa wasichana huu ni wakati wa kutumia juice hii kwani huweka mwili katika kiwango kizuri cha acid na base yaani ph na kusaidia ukuaji wa viungo vya mwili ikiwemo nywele zenye afya.

hupunguza cholestrol mwilini: utafiti unaonyesha beta sitisterol inayopatikana kwenye mmea huu inaweza kurudisha katika hali ya kawaida cholestrol nyingi inayokua imejaa mwilini, ambayo ni hatari sana na ndio chanzo kikuu vya magonjwa ya moyo.

inaongeza kinga ya mwili; juice hii inaondoa vimelea huru ndani ya mwili maarufu kama free radicals ambazo ni hatari kwa mwili kwani husababisha kansa. kimiminika hii kina vitamin e ambayo ni maalumu kwa kazi hiyo.

inatibu matatizo mbalimbali ya tumbo; kila mtu kwa wakati wake mwenyewe katika maisha hupata kiungulia, tumbo kusokota, kutapika ghafla, tumbo kuunguruma na kadhalika. juice hii hutuliza mihangaiko hiyo na husaidia sana katika kutibu madonda ya tumbo.

                                           jinsi ya kutumia;
mimina nusu glass ya juice hii ikiwa kawaida au baridi  na unywe mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni na moyo wako utakushukuru.

mwisho; juice hii unaweza ukanywa zaidi ya kiasi kilichotajwa kama una uwezo mkubwa wa kua na juice nyingi  nyingi zaidi lakini kiasi kilichotajwa hapo ndio cha chini kabisa kwa siku ili kiweze kukusaidia.
 DR ONESMO EDISON
0759913570
0673913571