Saturday, 17 October 2015

HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE KUKOSA HEDHI.


Wengi wanafahamu kwamba mwanamke akipata mimba hawezi kuziona siku zake za hedhi bila kujua kuwa ziko sababu nyingine zinazoweza kusababisha jambo hilo. Kwa kawaida mwanamke huacha kupata hedhi kitaalam huitwa Menopause anapofikisha umri wa miaka 42 -55 na kuendelea.
Leo nitazieleza sababu nje ya utaratibu huo wa kimaumbile unaoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).

MAABUKIZI YA WADUDU.
Maabukizi ya magojwa tofauti yaweza sababisha mwanamke asipate kuona siku zake.magojwa yale yana vuruga mfumo wa utoaji wa hormone katika mwili wa mwanamke. eg PID (pelvic inflamatory disease, gono etc
SIGARA Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.
 UNENE Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.Kitaalam hali hiyo inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani Sex homones.
ULEVI Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku.
KUTOKULA NYAMA Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao wamo katika hatari ya kukosa kuona siku zao za hedhi. Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari ya kupata saratani ya matiti. Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiiana kwa mwanamke. Hali hiyo husababisha tupu za mwanamke kuwa kavu, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
 USHAURI Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka ni vyema akaenda kumuona daktari ili afanyiwe uchunguzi na kama ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi.
Dr Onesmo Edison
0759913570
0673913571

No comments:

Post a Comment