Thursday, 15 October 2015
HAYO NDIO MAMBO KUMI YA SIRI AMBAYO HAYASEMWI KUHUSU JUISI ZA ALOE VERA.
Aloe vera sio mmea mpya masikioni mwa watu kwani umetumika kwa miaka mingi sasa kutibu magonjwa mbalimbali na kuzuia vifo vingi ambavyo vingesababishwa na magonjwa mbalimbali. huku kwetu afrika watu wanafikiri bidhaa zinazotokana na mmea huu adimu ni dawa tu kwa binadamu. lakini ni kosa kusema hivyo kwani dawa ni kitu ambacho ukitumia kinakutibu na kuacha baadhi ya sumu zake...lakini bidhaa za mmea huu ni virutubisho ambavyo vinakutibu na kukuzuia na magonjwa mbalimbali. kiufupi wenzetu huko nje wanatumia bidhaa hii kama sehemu ya chakula lakini sisi tunatumia tukiugua tu, huenda ni sababu ya ugumu wa maisha yetu lakini kama unaweza bidhaa hizi zisiishe ndani kwako.
leo naomba nikupe siri kumi kumi usizozijua za juice hii inayotokana na mmea wa alo evera ikiwa imetengenezwa bila kuwekewa kemikali hata moja.
kuondoa sumu mwilini: kama umeshawahi kuona mmea wa aloe vera yale maji yake ya ndani ni mazito kama mlenda hivi, kwa hiyo ukinywa juice yake haitoki haraka tumboni kama maji ya kawaida hivyo kutoka kwake taratibu kunaifanya inyonye sumu zilizoko kwenye mfumo wa chakula na mfumo wa damu ili kutoka nazo nje na kukuacha mpya.
hupunguza uzito; kuondoa sumu mwilini ni sawa na kufuta baadhi ya faili kwenye computer iliyojaa kwani computer hiyo itaanza kufanya kazi kwa haraka sana, hivyohivyo kwenye mwili sumu zikitoka mwili hufanya kazi kwa haraka sana na kupunguza mafuta yaliokua yameuelemea.
hulainisha choo; mara nyingi watu hupata choo ngumu sana kwa sababu ya kula vyakula visivyo na maji ya kutosha kama nyama nyingi na wanga bila kula matunda hivyo juice hii hulainisha na kusafisha njia ya choo kubwa, hii itakusaidia kupata choo kilaini sana.
ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari; kama unasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari juice ya aloe vera inasaidia sana kushusha sukari ya mwili na kukufanya uishi maisha safi sana.
matibabu ya magonjwa ya kinywa; utafiti unaonyesha juice hii huua bacteria wa mdomoni ambao huweza kusababisha magonjwa ya meno na ndio maana kuna dawa za meno zinatengenezwa kwa mmea huu.
hutibu magonjwa ya ngozi na chunusi; juice hii huupa mwili kiwango cha madini na vitamini za kutosha pia kuongeza maji mwilini, hii hulainisha ngozi yako na kukufanya ue na ngozi laini sana na yenye afya.
huongeza urefu wa nywele; kama unataka kua na nywele ndefu hasa kwa wasichana huu ni wakati wa kutumia juice hii kwani huweka mwili katika kiwango kizuri cha acid na base yaani ph na kusaidia ukuaji wa viungo vya mwili ikiwemo nywele zenye afya.
hupunguza cholestrol mwilini: utafiti unaonyesha beta sitisterol inayopatikana kwenye mmea huu inaweza kurudisha katika hali ya kawaida cholestrol nyingi inayokua imejaa mwilini, ambayo ni hatari sana na ndio chanzo kikuu vya magonjwa ya moyo.
inaongeza kinga ya mwili; juice hii inaondoa vimelea huru ndani ya mwili maarufu kama free radicals ambazo ni hatari kwa mwili kwani husababisha kansa. kimiminika hii kina vitamin e ambayo ni maalumu kwa kazi hiyo.
inatibu matatizo mbalimbali ya tumbo; kila mtu kwa wakati wake mwenyewe katika maisha hupata kiungulia, tumbo kusokota, kutapika ghafla, tumbo kuunguruma na kadhalika. juice hii hutuliza mihangaiko hiyo na husaidia sana katika kutibu madonda ya tumbo.
jinsi ya kutumia;
mimina nusu glass ya juice hii ikiwa kawaida au baridi na unywe mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni na moyo wako utakushukuru.
mwisho; juice hii unaweza ukanywa zaidi ya kiasi kilichotajwa kama una uwezo mkubwa wa kua na juice nyingi nyingi zaidi lakini kiasi kilichotajwa hapo ndio cha chini kabisa kwa siku ili kiweze kukusaidia.
DR ONESMO EDISON
0759913570
0673913571
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment